VIRUS 30

       CHAPTER 01
            

           
       Nimeamka asubuhi baada ya kusikia kelele."mh!! kuna nini kimetokea?" Nilijiuliza
Nikaamua kuinuka kitandani na kuchungulia dirishani nilishtuka nilichokiona watu wanakimbia ovyoovyo
   "Mh!!nini hiki tena??"nilijiuliza
Nikaenda kuwasha luninga ila ghafla umeme ukakatika "AGH!!!" Nilisema huku nikirusha rimoti ya luninga na kuivunja vipande kadhaaa 
  "Dah!!! Ama kweli hasira hasara sasa nimevunja remoti nitaangaliaje tena televisheni (luninga)?"nilijiuliza huku nikijiona mjina kwa kufuata hasira zangu 
Mara ghafla mlango wangu ukagongwa 
   "Ngo ngo ngo hodi!!!"mtu anaye bisha hodi alisema
   "Nani mwenzangu?"niliuliza kwa hofu tena maana niliona watu waking'atana yaani kama mazombi wa kwenye muvi
   "Ni...ni mimi JACOB fungua chapa maana huku nje hali si shwari" alisema ulyule mtu anayebisha mlango
   "Ok poa nakuja kukufungulia" nilimjibu huku nikivaa track suti yangu na kwenda  kumfungulia 
   "Asante man yaani huko nje sio poa kabisa" alisema jacob
    "Dah!! Poa man karibu kaa hapo kwani huko nje kuna nini maana makelele yake sio poa kabisa "nilimwambia
   "Man watu wamepata huko nje wanang'ata watu wamekuwa kama vichaa yaani acha tu" Jacob alijibu nami wakati huo ninawasha redio kusikia nini kimejiri
  "Ugonjwa usiojulikana umezuka duniani ukiwa inaangamiza mamia elfu ya watu na wengine kuwafanya kama vichaa.Ni jambo lisilo la kawaida maana ugonjwa huu haujulikani umeanzia wapi ila inaonekana kuwa na dalili zilezile za covid 19 ya miaka kumi na moja iliyopita ila huu uko more advanced.kwa ushauri subiri nyumbani.Na kwa hapa nchni kwetu Tanzania tunakuomba isitoke nyumbani tena subiri mpaka msaada utakapopatikana."alisema yule mtangazaji na akaongezea kuwa tutakupa taarifa kuhusu dalili na jinsi unavyoweza kusambaa"
  "Mh!!!man hali sio nzuri man"nilisema 
   "Ndio man sio poa kabisa yaani watu wamechanganyikiwa"alisema Jacob 
   "Oy umeme umerudi vipi kuhusu tv?"aliuliza Jacob
  "Dah!!!man si nilivunja rimoti ila wewe washa tu ukontro kwa kawaida"nilimjibu naye akawasha runinga na kuiset kwenye chaneli aliyoitaka na mimi nikaenda kupika chai.Baada ya kama saa moja nikiwa namalizia kupika chapati.
   "Habari muhimu kwa sasa.Waziri wa Afya Mheshimiwa Magreth Samson ameleta taarifa na kuelezea kuhusu ugonjwa mpya uliozuka duniani" alizungumza mwandishi wa habari 
    "Habari ya saizi watanzania wenzangu leo ninataarifa ya kuhusu mlipuko wa ugonjwa hatari ambao haujulikani umetokea wapi na ugonjwa huu umelipuka kwenye hospitali kubwa. Dalili ya ugonjwa huu ni hasira kupitiliza,kubwa na njaa na kuwa na tamaa ya kula nyama ya mbichi pia wanapenda kuwinda nyama yake mwenyewe. Dalili ya kwanza hutokea baada ya masaa mawili mtu huanza kuwa na homa kali sana  na joto la mwili huongezewa ila baada ya masaa matano mgonjwa hupata njaa kali na pia hasira kutokana na kutoweza kushiba ugomvi" alisema waziri huku alifungua ukurasa mpya kwenye karatasi yake.
  " Sasa tunafanyaj sasa  maana tiyari mambo yamebadilika" alisema Jacob 
   "Tahadhari ni kwamba ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya kung'atwa na pia  kwa njia ya damu" alisema waziri ila muda huo ghafla kelele zinasikika kwenye redio huku walinzi wa waziri wakisema    "kuheshimiwa twende sehemu salama"
    "Duh hali sio hali hapa yaani hatufiki nje"alisema Jacob huku akiniangalia mimi nilikuwa na mshtuko tu.


Post a Comment

Previous Next

Ads before post

Ads after post